SUGU APATA MTOTO WA KIUME, AMPA JINA LA JAY-Z

MBUNGE wa Mbeya mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mchumba wake, Happyness Msonga wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la rapa maarufu wa Marekani, Shawn Carter maarufu kama Jay Z.

 

Sugu ambaye pia ni rapa mkongwe hapa Bongo, ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika maneno haya.

Tumempa mtoto wetu jina Shawn joseph Mbilinyi… SHAWN (Tamka SHON), lina maana ya zawadi kutoka kwa Mungu  ( A GIFT FROM GOD). Pia ni katika kumuenzi msanii na mfanyabiashara maarufu duniani JAY-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER. Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha. Asanteni sana… #JONGWE #MVMP #MisutiKabatini,” ameandika Sugu.

 

Loading...

Toa comment