The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars Yaipiga Equatorial Guinea Bao 2-1 Taifa

TANZANIA imeanza vyema mbio za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.


Haukuwa ushindi mwepesi, kwani hadi mapumziko, tayari Equatorial Guinea walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa Sassuolo ya Italia, Pedro Mba Obiang dakika ya 15 akimtungua kipa mkongwe wa Tanzania, Juma Kaseja kwa shuti la mbali.

Kikosi kilichanza cha Stars kilikuwa na Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Kelvin Yonda, Hassan Kessy, Bakari Mwamnyeto, Salum Abubakar, Mbwana Samatta, Simon Msuva, Mohamed Hussein, Farid Mussa na Mzamiru Yassin.

Comments are closed.