The House of Favourite Newspapers

Tanasha Donna na Diamond Platnumz ‘Mondi’ Wazua Gumzo, Zari Atajwa

0
Tanasha Donna

ETI umewahi kusikia uhawara hauna talaka? Kwa mbaliiii sanaaaa inawezekana ikawa kweli! Maana ujio wa mwimbaji Tanasha Donna kutua jijini Dar es Salaam na kujiachia kimahaba nyumbani kwa mzazi mwenzake Diamond Platnumz ‘Mondi’ kumezua gumzo.

Ukisikia watu wanaimba: “Moto, moto, motooo! Wewe itikia “Motoooo” ili maisha yaendelee.

Katika video zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Tanasha anaonekana akistarehe kwenye kochi nyumbani kwa Diamond pamoja na mwanawe. Tanasha ambaye ni msanii na mtangazaji raia wa Kenya na Mondi wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume katika uhusiano wao wa muda mfupi uliovunjia Februari 2020.

Diamond Platnumz ‘Mondi’ akiwa na mtoto aliyezaa na Tamasha.

Baada ya penzi lao kufa maana hawakuwa wameoana Tanasha alirejea kwao na alipohojiwa na Jarida la True Love alieleza machungu aliyokutana nayo kwenye uhusiano wake na Diamond kiasi cha kufungasha virago.

Alipoulizwa kama atarudi  kwa Diamond, alisema: “Kwa sasa, akili yangu imekuwa na kiwewe hadi sijui kama naweza.” Akaongeza: “Hakuna uhusiano tena kwa sasa, labda baada ya miaka miwili hadi mitatu, sasa nimeolewa.” Nukuu hiyo huenda Tanasha alijua kuwa maumivu aliyodai kuyapata kwenye uhusiano wake na Mondi yangepoa baada ya miaka mitatu maana tayari imetimia na yeye amelegeza kamba.

Katika kuonesha kuwa Tanasha kalegea kwa ‘Simba’ tayari amemfungulia mlango wa mawasiliano msanii huyo wa Bongo aliyokuwa ameyafunga kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye ulimwengu wa mitandao tayari kumezuka fununu kwa wawili hao wanapanga kufunga ndoa baada ya kusameheana katika yote.

Mwanadada Zarina Hassan ‘Zari’

Hata hivyo, video na picha mpya za Mondi na Tanasha zinazoenezwa mitandaoni zimekuwa mwiba mchungu kwa msanii Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ kwani wengi wanamcheka kwamba hana lake tena.

Imekuwa ikidaiwa mara kadhaa kwamba Mondi anatoka kimapenzi na msanii wake Zuchu ambaye anatumikia Lebo ya muziki ya WCB. Ukweli wa hili uko mioyoni mwa wawili hao lakini mara kadhaa wamekuwa wakikanusha kuwa siyo wapenzi bali wanaishi kama kaka na dada.

Kama wasemavyo Waswahili shavu moja likiunguzwa na uji jingine lijiandae kupokea moto basi mwanadada Zarina Hassan ‘Zari’ naye haponi maumivi ya ufufuo wa penzi la Mondi na Tanasha. Ifahamike kuwa Zari kwa upande wake alikuwa mpenzi wa Mondi na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili. Inaelezwa kuwa ingawa Zari haoneshi kuwewesekea penzi la mzazi mwenzake Mondi lakini wachunguzi wa mambo wanasema anateseka.

Wanasema kitendo cha mwanamke huyo kuposti nyimbo za Harmonize katika siku za hivi karibuni ni ushahidi kuwa anatupa kijembe wa Mondi na kuonesha bado anampenda. Ni hakika yanasemwa na yatasemwa mengi Gazeti la Ijumaa linasubiri kuona nini kifuatacho baada wawili hao kufufua penzi lao? Maana kuu katika hili ni kwamba Mondi haaminiki kwani mara kadhaa amekuwa akiahidi kuoa lakini mpaka leo bado bachela licha ya kuhusishwa kimapenzi na wanawake lukuki hadi watatu kuzaa nao.

Stori; RICH RICHARD, GPL

MO DEWJI APASUA JIPU; KUNA WATU NDANI YA SIMBA WANAKWAMISHA, ANGEKUWA MWINGINE ANGESHAJITOA!

Leave A Reply