The House of Favourite Newspapers

TANASHA: MONDI KIDOGO ANIPE UCHIZI

MPENZI wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch amesema kuwa, ilibaki kidogo apate uchizi baada ya kutoka na msanii huyo.

 

Akizungumza na Citizen TV katika Kipindi cha 10 Over 10, Tanasha ambaye pia ni msanii wa muziki na Mtangazaji wa Radio NRG ya nchini humo alisema kuwa alipoanza kuwa na uhusiano na Mondi yalizuka maneno mabaya kwake ambayo yalitaka kumpa uchizi.

 

“Mwanzoni maneno hayo nilichukulia kawaida tu. Yakaanza kunifanya kupata msongo wa mawazo, lakini nilika-biliana nayo. Kama Yesu ananichukia jinsi nilivyo siwezi kuwa…” alisema Tanasha.

 

Mondi na Tanasha walianza kutoka rasmi kimapenzi Novemba, 2018. Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza katika klabu ya usiku 2016, lakini hawaku-weza kuwa karibu hadi walipo-onana 2018.

LIVE: IBADA ya MAZISHI ya MENGI, WAZIRI MKUU AWASILI KANISANI

Comments are closed.