visa

Tanasha: Sina Usista Duu Kwenye Kulea

MASTAA wengi wanapokuwa wanalea wanaweka ustaa mbele na kusahau kwamba washakuwa mama, ishu hizo ndizo hataki kuzisikia kabisa mpenzi wa sasa wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Tanasha Donna na kusema usista du hana muda nao kwenye malezi.

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Tanasha alisema kuwa kama mwanamke atafanya kama vile walikuwa wakifanya wazazi wa kizamani, wanalea na kunyonyesha mpaka umri unaostahili.

“Mimi sidhani kwa kweli kama nitaweka usistaa duu kwenye malezi kwa sababu nitakuwa siyo mama halisi nataka nilee kizamani kabisa kama wazazi wetu walivyotulea na nitanyonyesha mpaka mwisho,” alisema Tanasha ambaye anatarajia kujifungua hivi karibuni.
Toa comment