The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Paroko Mbiku UDSM Afariki Dunia

0

Wapendwa Mapadri, Mashemasi, Watawa na taifa lote la Mungu, Kristo.

 

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Monsinyori Deogratias Hukumu Mbiku wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Chuo Kikuu.

 

Monsinyori Mbiku amefariki tarehe 04 Aprili 2021 saa 12:45 jioni katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa, DSM, alipokuwa akitibiwa. Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu.
Naomba tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni.

 

ASANTENI.
+ Jude THADDAEUS Ruwa’ichi,
Askofu Mkuu wa DSM.

Leave A Reply