The House of Favourite Newspapers
gunners X

Tasnia ya Filamu Yapoteza Mwigizaji Laisa, Msiba Wathibitishwa – Video

0

Tasnia ya filamu nchini imepokea taarifa za msiba wa Laisa, ambaye alikuwa mfanyabiashara na muigizaji katika BongoMuvi. Taarifa hizo sasa zimethibitishwa rasmi baada ya mazungumzo na mfanyabiashara na mtu wa karibu wa marehemu, @sophie_amelowa, ambaye amekiri kuwa msiba huo umetokea leo.

Kwa mujibu wa Sophie, tasnia imepoteza kijana aliyekuwa na juhudi, mipango, na malengo mengi ndani ya sanaa na biashara. Amesema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwa wale waliomfahamu na kushirikiana naye.

Chanzo cha Kifo

Chanzo cha kifo cha Laisa kinatajwa kuhusishwa na tatizo la presha pamoja na msongo wa mawazo, ingawa taarifa za matibabu kutoka kwa madaktari bado hazijatolewa rasmi. Familia na watu wa karibu wanatoa wito kwa umma kusubiri taarifa sahihi zaidi kutoka kwa wahudumu wa afya na ndugu.

Leave A Reply