The House of Favourite Newspapers

Timu 16 kushiriki CECAFA, Simba na Yanga ndani

0

TIMU za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa zitapata nafasi nzuri ya kujiandaa na msimu mpya kwa kucheza na timu za Zambia, Sudan, Rwanda, Kenya na Uganda.

Habari za uhakika zinaonyesha Yanga mabingwa wa ligi, Azam FC, Simba na Coastal Union zitashiriki michuano ya Cecafa dhidi ya timu kutoka katika mataifa hayo.

Cecafa ni Baraza lenye wanachama 12 ikiwemo Zanzibar na mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Tanzania ikiwa ni fursa kwa timu za Tanzania kushiriki pia.

Timu hizo nne zitakazoshiriki Caf Champions na Caf Confederation Cup zitacheza dhidi ya Al Hilal, Al Merreikh na Hai Ak Wadi za Sudan, Red Arrow ya Zambia na TP Mazembe ya DRC.

Michuano hiyo ambayo itakuwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya zitashirikisha timu 16 na itapigwa Tanzania.
Ikumbukwe kwamba Yanga na Azam FC hizi ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Coastal Union ni kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Timu nyingine ni Nyasa Big Bullets ya Malawi, SC Villa ya Uganda, APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Vital’O (Burundi), JKU (Zanzibar) na El Merreikh Bentiu (Sudan Kusini).

 

Leave A Reply