The House of Favourite Newspapers
gunners X

Trump Atangaza Msimamo Mkali Greenland Lazima Ichukuliwe

0

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema taifa hilo lipo tayari kuhakikisha linachukua udhibiti wa kisiwa cha Greenland kwa njia yoyote ile, iwe kwa makubaliano au kwa nguvu, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni ya muhimu kwa usalama wa taifa la Marekani.

Trump ametoa kauli hiyo siku ya Ijumaa alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari, ambapo alieleza kuwa iwapo Marekani haitachukua hatua mapema, basi nchi hasimu kama China au Urusi zinaweza kuichukua Greenland, jambo ambalo amesema ni tishio kubwa kwa usalama wa Marekani.

“Kwa sasa tunakwenda kufanya jambo kuhusu Greenland, iwe wanapenda au hawapendi. Tusipofanya hivyo, Urusi na China watachukua nafasi hiyo, na hatutakuwa na China au Urusi kama majirani,” amesema Trump.

Kwa mujibu wa Trump, sababu kuu ya Marekani kuhitaji Greenland ni masuala ya kiusalama, akibainisha kuwa uwepo wa China au Urusi karibu na mipaka ya Marekani unaweza kudhoofisha usalama wa taifa hilo.

Kauli hiyo imeendelea kuzua mjadala mkubwa kimataifa, hasa ikizingatiwa kuwa Greenland ni eneo lenye umuhimu mkubwa wa kimkakati, rasilimali asilia na nafasi ya kipekee katika masuala ya kijeshi na usalama wa dunia.

BALAA la TAIFA ANALOLITAKA TRUMP – KUMBE LINA MADINI ADIMU – ANATAKA KUJARIBU TENA KULINUNUA…

Leave A Reply