The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Apasuliwa Tena Mguu, Atoa Kauli

MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.

 

Upasuaji huu utakuwa ni wa 20 tangu alipoanza kutibiwa, baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka jana.

 

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu. 

ALICHOKIANDIKA LISSU KWENYE INSTAGRAM ACCOUNT YAKE  ASUBUHI HII

Comments are closed.