The House of Favourite Newspapers

Ufuta Unavyotibu Kisukari, Saratani!

UFUTA au kitaalamu Sesamum indicum, hustawi na hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na sehemu ya mkoa wa Ruvuma, Tunduru. 

Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu

Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shambulio la moyo, kuimarisha mmeng’enyo wa chakula, huondoa lehemu, huboresha ngozi, huondoa na kukinga saratani na kuongeza damu. Pia ufuta huzuia mwili kuharibiwa na mionzi na mionzi ya jua, hulinda ini dhidi ya madhara ya pombe, hung’arisha ngozi na kuimarisha afya ya macho.

Faida nyingine kuwa ni kuzuia maradhi ya kinywa. Pia huimarisha mfumo wa upumuaji, lishe kwa watoto wadogo na kuimarisha afya ya nywele na hivyo kuzuia tatizo la nywele kunyonyoka na kuota nywele kwa wale wenye uhaba au kutoota nywele.

Hiyo ni kutokana na aina mbalimbali za virutubisho vilivyomo katika mbegu za ufuta kama vile, protini, mafuta, madini kadhaa kama ya kopa, kalishiamu (calcium), chuma, zinki, fosforasi, manganizi, magineziamu na thiamine.

KISUKARI:

Ufuta huzuia na kutibu ugonjwa huo kutokana na mbegu zake kuwa na madini ya magneziamu ambayo yakiwa mwilini huzuia visababishi vya sukari kama vile tatizo la insulini na kongosho kutofanya kazi ipasavyo. Pia mafuta ya ufuta huimarisha kuta za plasma na hatimaye kuwa na uwezo zaidi wa kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu.

KUKOSA CHOO, SARATANI

Mtu mwenye matatizo ya kukosa choo au choo kigumu, anapaswa kula kwa wingi ufuta kutokana na virutubisho hivyo kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kufanya hali hizo kutoweka na kuondokana na tatizo la ugonjwa wa bawasiri.

Kuhusu ugonjwa wa Saratani, mbegu za ufuta zina misombo (compounds) kama vile asidi aina ya phytic madini ya maginesiamu na phytosterols ambayo kwa pamoja huukinga mwili na kuondoa sumusumu zinazosababisha saratani. Ufuta pia ni tiba ya matatizo yanayokabili kinywa.

Kwa miaka mingi sasa watu wa kabila la Ayurveda huko barani Asia, wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama tiba na kinga ya matatizo ya kinywa ikijumuisha meno, fizi na kingo za mdomo au kinywa.

SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA), MATATIZO YA UZAZI, KUONDOA KITAMBI

Ufuta hutibu pia matatizo ya moyo na shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambapo mara baada ya kula ufuta hushuka na kuwa la wastani kwa muda mfupi ikiwa matumizi yake yatazingatiwa.

Ufuta huweza kuimarisha moyo na kuulinda usishambuliwe na magonjwa ikiwa ni pamoja na kushusha ‘presha’ ya juu kutokana na virutubisho hivyo.

MATATIZO YA FIGO, KIBOFU…

Ufuta ni tiba muhimu katika tiba ya figo ikiwemo kuondoa mawe kwenye figo na matatizo ya kibofu. Pia una uwezo wa kutibu kipindupindu na kuzuia kuhara, kuweka sawa homoni zinazosababisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kwenda sawa.

Huongeza nguvu kwenye mifupa na kuimarisha misuli mwilini kutokana na kirutubisho cha Kalishiamu kilichomo. Huzuia na kutibu maumivu ya tumbo ya ghafla.

Ufuta pia ni tiba nzuri kwa matatizo ya mfumo wa upumuaji kwani virutubisho vilivyomo huyakinga mapafu dhidi ya hewa chafu na magonjwa yanayoambata na kusababisha mfumo wa hewa kutokuwa mzuri.

MATATIZO YA INI NA MACHO

Mtaalamu mwingine wa tiba lishe, Dk. Josh Axe wa nchini Marekani anasema kupitia kitabu chake cha Eat Dirt kuwa ufuta hulinda ini dhidi ya magonjwa.

Hiyo ni pamoja na kulifanya ini kuwa na uwezo wa kufanya kazi ipasavyo na kuliepusha na magonjwa hasa ikiwa limeathiriwa na pombe kwani ufuta huondoa sumu zilizomo zinazotokana na matumizi ya pombe.

Comments are closed.