The House of Favourite Newspapers

Ulinzi Waongezwa Kambi Ya Yanga Kuelekea Mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika

0

KUELEKEA mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga imeongeza ulinzi katika kambi yake waliyoiweka huko Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar.

Yanga inatarajiwa kuikaribisha USM Alger katika mchezo wa kwanza wa fainali utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar kabla ya kurudiana Juni 3, mwaka huu huko Algeria.

Katika mchezo huo Yanga wanahitaji ushindi wa mabao zaidi ya matatu ili wawape ugumu wapinzani wao watakapokuwepo ugenini katika mchezo wa marudiano.

Taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, kambini huko haitajiki kiongozi yeyote zaidi ya wachezaji na benchi la ufundi pekee ili kuongeza utulivu.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kikosi hicho mara baada ya juzi kurejea Dar, wakitokea mkoani Dodoma kwa ndege moja kwa moja kiliingia kambini tofauti na awali walikuwa wakipewa mapumziko ya siku moja hadi mbili kwa ajili ya kwenda kusalimia familia zao.

Aliongeza kuwa hakuna mchezaji yeyote aliyepewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwake, lengo kocha Nasreddine Nabi apate muda wa kuwapa mbinu za kiufundi zitakazowawezesha kutwaa taji hilo.

“Katika kuelekea michezo hiyo miwili, tunafahamu kabisa wapo baadhi ya viongozi wa tu na Serikali watataka kwenda kambini kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji kwa lengo la kuwapa hamasa.

“Hivyo hatutaki hilo litokee, na badala yake tumezuia watu kwenda kambini kwa lengo la kumpa utulizu kocha wa kukiandaa kikosi chake kwa siku hizi tano.

“Kitendo cha viongozi kwenda kambini kila wakati kutawavuruga wachezaji na badala ya kucheza kwa presha kubwa katika michezo hii miwili ya fainali,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumza hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe kuzungumza hilo simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa.

STORI NA WILBERT MOLANDI

YANGA WAELEZA NAMNA ya KUZIPATA TIKETI za BURE ZILIZONUNULIWA na VIONGOZI na WADAU…

Leave A Reply