
URUSI imesema haitamruhusu balozi wa Marekani kumtembelea mwandishi wa habari wa Marekani aliyezuiliwa nchini humo Evan Gershkovich
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov mwishoni mwa wiki iliyopita alilalamikia Marekani kwa kukataa kuwapa visa waandishi wa Urusi waliotarajiwa kwenda naye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Taarifa ya wizara hiyo imesema uuamuzi huo unafuatia kile ilichokitaja kama uamuzi wa kichokozi wa Marekani na kuonya juu ya hatua nyingine za kisasi ambazo bado zinaandaliwa.
Gershkovich alikamatwa nchini Urusi mwezi uliopita, kwa madai ya kufanya ujasusi.