The House of Favourite Newspapers

VEE MONEY AMFUNGUKIA JUX

BAADA ya maneno mengi kuendelea kusambaa mitandaoni kuwa penzi la mwanandada anayefanya poa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Juma Khalid ‘Jux’ limevunjika na kila mmoja anafanya maisha yake, hatimaye mrembo huyo ametoa ya moyoni.

 

Mara kadhaa penzi la wawili hao limekuwa likiripotiwa kuachana kisha kurudiana, jambo linalowapa sintofahamu mashabiki wao wa muziki kwani wamekuwa wakiwavutia sana, hata hivyo ili kupata undani wa madai hayo, Risasi Vibes lilifanya mahojiano na Vee Money.

 

“Hivi kwa nini watu wanapenda kufuatilia maisha ya watu jamani, halafu kitu ambacho huwa sipendi kabisa kukizungumza ni kuhusu hayo mambo, hebu tuzungumzie ishu za kazi basi, kwa sababu mimi na Jux hatuna tatizo lolote,” alisema Vee Money

Comments are closed.