The House of Favourite Newspapers

Video: Kamati ya Hamasa Yawaita Mashabiki Taifa Kesho

Kamati ya hamasa ya Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars  leo Novemba 14, 2019 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Haji Manara, imewamewaomba wa Tanzania kwenda kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuisapoti Taifa Stars itakapokuwa inavaana na Guinea ya Ikwetwa kwenye mchezo wa kwanza wa kundi J kutafuta nafasi ya kufuzu Mashindano ya Afrika (Afcon) yatakayofanyika nchini Cameroon 2021.

 

Wakizungumza na Waandishi wa habari kwenye kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya Sea Cliif, jijini Dar es salaam kamati hiyo imewaomba wa Tanzania kujitokeza kwa wingi wakiwa wamevalia Jezi zao za taifa ikiwa ishara ya kuiunga mkono timu hiyo.

 

Kwa upande wake katibu wa Shirikisho la soka Nchini TFF Willifred Kidao amewaeleza wa Tanzania kuwa wachezaji wapo katika Hali nzuri kuelekea katika mchezo wa hapo kesho.

Baada ya mchezo huo, Stars itakuwa na mchezo mwingine Novemba 19 wakicheza ugenini dhidi ya timu ya Taifa ya Libya.

Comments are closed.