The House of Favourite Newspapers

VILIO TUPU! KUAGWA KWA MWANAKWAYA ALIYEUAWA GESTI – PICHAZ

VILIO, simanzi na mazjonzi vimetawala miongoni mwa waombolezaji leo Jumamosi, Septemba 8, 2018 wakati wa kuaga mwili wa mwanakwaya Mariam Charles (25) anayedaiwa kuuawa na mchumbaake.

Jeneza lenye mwili wa marehemu.

Mwili wa Mariam umeagwa kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la African Inland lililopo Chang’ombe Jijini Dar es Salaam huku ibada ikihudhuriwa na umati mkubwa waombolezaji wakiwemo wanakwaya wenzake.

Wazazi wa marehemu wakiwa kwenye ibada ya kuaga.

Mwanakwaya huyo ambaye alikuwa mkazi wa Keko Furniture, wilayani Temeke jijini Dar alikutwa ameuawa kwenye Gesti ya East London, Mtaa wa Kwa Hamad Bonge, Temeke, Septemba 5, mwaka huu huku mchumba wake aliyetajwa kwa jina la Frank ambaye amehusishwa na mauaji hayo.

Wanakwaya wakiimba wakati wa ibada ya kuaga.

Baada ya ibada na kuagwa, mwili huo umezikwa leo katika makaburi ya temeke.

Waombolezaji wakiwa kwenye ibada.

 

Mama wa marehemu akilia kwa uchungu.

 

Wanakwaya wenzake na marehemu wakilia.

 

MWANAKWAYA ALIYEUAWA GESTI, FAMILIA YASIMULIA MAZITO – VIDEO

 

 

 

Baba mzazi akiaga.

 

Mama wa marehemu akiaga mwili wa mwanaye.

 

 

Mwili ukitolewa kanisani kupelekwa makaburini.

Picha na Richard Bukos | GPL

Comments are closed.