The House of Favourite Newspapers

VINARA TUSUA MAISHA WAKABIDHIWA ZAWADI, SPOTI EXTRA LATIKISA

Bholen Kilimba (kulia), akikabidhiwa zawadi ya pikipiki na Judith Mlwale wa Global TV.

Yametimia! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kukabidhiwa zawadi kwa washindi wa droo za mwisho za Shindano la Tusua Maisha, zoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa Gazeti la Spoti Extra Toleo la Ahamisi.

Kilimba akiwa juu ya pikipiki yake

 

Mpango mzima ulikuwa ni kwenye Uwanja wa Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam ambapo washindi waliokuwa wakisubiri kwa hamu zawadi zao, walikabidhiwa na hivyo kumalizika rasmi kwa Shindano la Tusua Maisha na Global lakini pia kuanza kwa shindano lingine ndani ya Gazeti la Spoti Extra.

Hamis Mohamed (kulia), akikabidhiwa zawadi ya dinner set na Jimmy Haroub

 

Waliokabidhiwa zawadi zao ni Bholen Kilimba wa Tukuyu, Mbeya aliyefunga safari kutoka Mbeya mpaka Dar es Salaam kupokea zawadi yake ya pikipiki mpya, Halima Jabir wa Mbagala aliyesindikizwa na wazazi wake kupokea pikipiki yake na Hamis Mohamed wa Kinondoni aliyeondoka na dinner set.

Vaileth Mtilega (kushoto), akikabidhiwa zawadi ya jezi na Mc Chaku

 

Wengine ni Vaileth Mtilega wa Kiwalani aliyeondoka na jezi na Eliuter Ndunguru wa Manyoni aliyewakilishwa na Odilia Ndunguru kupokea jezi zake.

 

Burudani mbalimbali zilipamba tukio hilo lililokusanya umati mkubwa ambapo pia wasomaji wa Gazeti la Spoti Extra walipata bahati ya kujishindia zawadi mbalimbali za papo hapo kutokana na kujaza kuponi zilizopo ndani ya gazeti hilo, ambalo sasa litakuwa likitoka mara mbili kwa wiki, Alhamisi na Jumapili kwa bei ya shilingi 500 tu.

Halima Jabir (kulia) akikabidhiwa zawadi na Anthony, Afisa Masoko wa Global Publishers

 

Kabla ya tukio hilo, asubuhi ya leo, Septemba 20, viongozi mbalimbali na wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers waliingia mitaani kuuza gazeti jipya la Spoti Extra Toleo la Alhamisi lililopokelewa kwa kishindo na wasomaji wake, nchi nzima.

Halima Jabir akiwa juu ya pikipiki aliyoshinda
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Global Publishers
Wasomaji wakipewa maelezo na maafisa masoko wa Global Publishers, juu ya gazeti jipya la Spoti Extra Alhamisi
Burudani zikiendelea katika Uwanja wa Bakhresa, Manzese jijini Dar
Mratibu wa Shindano la Tusua Maisha na Global, Aziz Hashim akifafanua jambo
Msomaji akipewa maelekezo ya namna ya kujaza kuponi
Washindi wa Tusua Maisha wakifuatilia kwa makini maelekezo
Aziz Hashim akikabidhi zawadi ya fulana kwa mshindi wa papo kwa hapo.
Jimmy Haroub akitoa maelezo kwa msomaji
Afisa Masoko wa Global Publishers, Anthony akifafanua jambo
Mratibu wa Burudani wa Dar Live, Zagalo akikabidhi zawadi ya jezi kwa mshindi

Comments are closed.