The House of Favourite Newspapers

Viongozi Chadema Wasota kwa RPC Ruvuma

0
Viongozi wa Chadema (Picha na mktaba).

 

Viongozi tisa wa Chadema akiwamo Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji wameripoti kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma leo saa 4 asubuhi kama walivyotakiwa kufanya.

Akizungumza ofisini kwake leo Jumanne, Julai 18, kamanda huyo, Gemini Mushi amesema viongozi hao wameripoti ofisini kwake leo asubuhi na mpaka sasa wapo hapo wakisubiri jalada la kesi yao.

Ruvuma: Viongozi wa Chadema Waliokamatwa, Waachiwa Huru

Imeelezwa kuwa jalada lao lipo kwa wakili wa serikali mfawidhi mkoa wa Ruvuma. Viongozi hao walikamatwa na Polisi Julai 15, kwa madai ya kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

 

Pamoja na Dk Mashinji, wengine waliokamatwa ni mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, Philberth Ngatunga ambaye ni Katibu  wa Chadema Kanda ya Kusini, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma, Erineus Ngatura  na  Katibu wa Chadema mkoa wa Ruvuma, Delphin Gazia.

 

Wengine ni Zubeda Sakuru, mbunge viti maalum mkoa wa Ruvuma (Chadema), Sang’uda Moses, mkuu wa Oganaizesheni na Mafunzo (Chadema), Curthberth Ngwata Mwenyekiti Wilaya ya Nyasa pamoja na Charles Makunguru ambaye ni Katibu Mwenezi Wilaya ya Nyasa.

Chadema Yatangaza Vita na CUF ya Lipumba

Leave A Reply