The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Wanafunzi Zaidi ya 20 na Walimu Wao Wafariki Ajalini Karatu

2

ARUSHA: Wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao (idadi haijafahamika) wamefariki dunia baada ya basi la wanafunzi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.

Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa wanafunzi hao ni wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & Primary School English Medium iliyopo Arusha, walikuwa wakienda Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu.

Mazingira ya shule hiyo.

Inaelezwa kuwa ni watoto wanne(4) pekee ndiyo wanasadikiwa kuwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeru wa ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha na kusema atatoa taarifa kama ajali hiyo imesababisha madhara akifika eneo la tukio.

Global Publishers imefanya mazungumzo na Mkuu wa Shule hiyo ambaye hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa hawawezi kufahamu idadi kamili ya waliopteza maisha mpaka baadae ambapo shughuli ya uokoaji na kuhifadhi miili itakapokamilika ndipo watatoa taarifa tasmi.

======

UPdates

Habari za hivi punde kutoka Hospital ya Lutheran Karatu maiti zilizopokelewa hapo hospitali ni maiti 32 miongoni mwao walimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wavulana ni 11 na wasichana 18 nakufanya jumla hiyo ya maiti 32 pamoja na majeruhi 6 mbao wanaendelea na matibabu.

Taarifa zaidi kukujia baadae.

Wanafunzi wa shule hiyo.

Ajali ya Treni na Daladala Yawagusa Wengi, Kamanda Sirro Afunguka

2 Comments
  1. […] wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamadi jana ametoa salam za rambirambi kutokana na vifo vya wanafunzi 29 , walimu 2 na dereva mmoja vilivyotokea […]

  2. […] ajali ya gari Arusha ambapo serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali. […]

Leave A Reply