The House of Favourite Newspapers

Wanandoa Wanunua Video CD Feki Iliyosainiwa na Michael Jackson

0

ht_michael_jackson_autograph_em_160819_4x3_992WANANDOA wawili North Caroline, Marekani, wamenunua kanda ya video (VCD) iitwayo “Bad”, ambayo wanaamini ilitiwa saini na mwanamuziki hayati Michael Jackson,  kwa senti 25 tu katika duka moja.

 Amber na Michael Hernon of Concord, walishangaa baada ya kuona saini ya mwimbaji huyo iliyokuwa ndani ya kasha la kanda hiyo.  Saini hiyo haijathibitishwa na wawili hao hawana mpango wa kufanya hivyo hadi watakapoiuza.

“Nilishangaa nilipolifungua kasha hilo,” Amber aliliambia shirika la habari la ABC News kuhusu ugunduzi wao huo kwenye duka liitwalo Heavenly Treasures, “kisha nikamwambia Michael kwamba lilikuwa limesainiwa.  Kwa jinsi  nilivyokuwa nikimwambia, alijua nilikuwa namaanisha nilichokuwa nakisema.”

Waliiona sain ihiyo baada ya kufungua kasha la kaseti hiyo iliyokuwa na picha za Jackson akicheza na wakamwonyesha pia mtoto wa kiume wa Amber mwenye umri wa miaka 10 ambaye ni mpenzi mkubwa wa mwanamziki huyo.

Japokuwa saini hiyo inaonekana inafanana na ya Mfalme Pop huyo kutokana kuiona kwenye intaneti, hawataki kuanzisha mabishano yoyote kama ni ya kweli au si ya kweli, bali wataithibitisha tu iwapo watataka kuiuza.

Leave A Reply