Wapinzani wa Simba kutua Ijumaa

WAPINZANI wa Simba UD do Songo wanatarajia kutua nchini siku ya Ijumaa tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba. Simba inatarajiwa kurudiana na Songo, Agosti 25, ambapo katika mchezo wa awali uliochezwa Msumbiji timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano na Songo yamekamilika na wapinzani wao watafi ka Ijumaa.

“ Viingilio katika mchezo wetu na UD do Songo vitakuwa elfu 5000 kwa mzunguko VIP B na C itakuwa elfu 15,000, wakati VIP A itakuwa ni 30,000 na Platinum itakuwa na viingilio viwili ambavyo ni 100,000 na 150,000. “ UD do Songo wanatarajia kuwasili siku ya Ijumaa.

 

“ Tiketi zitaanza kuuzwa Alhamisi, na mfahamu tu kwamba Simba ndiyo inaongoza kuingiza mashabiki wengi Afrika, nadhani CAF wanaweza kutupa tuzo msimu huu,” alisema Manara.

 

Wakati huohuo, Manara amezungumzia juu ya nafasi yake ndani ya Simba kwa kusema kuwa yeye ndiye msemaji wa klabu hiyo lakini pia hatokaa hapo milele, na ikitokea mtu mwingine akipewa nafasi hiyo, apewe ushirikiano.


Loading...

Toa comment