MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepokea makontena ishirini kutoka kwa Watanzania waishio Marekani yakiwa na vifaa mbalimbali vya samani za ofisi za walimu wa mkoa huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda amewashukuru Watanzania hao waishio ughaibuni kwa msaada huo na kuahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa.
Makonda aliowaomba wadau wa mradi huo wasaidie kulipia gharama za usafirishaji wa samani hizo na gharama zingine za ndani ili ziweze kupatikana na kutumiwa sehemu husika. Wakati huohuo, Benki ya Walimu – Mwalimu Commercial Bank – imelipia baadhi ya makontena hayo.
Naye makamu mwenyekiti anayesimamia mradi huo, Solomon Urio, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa za kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia shughuli za kimaendeleo.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.