The House of Favourite Newspapers

Wawa arejea, aiwahi Singida United

Beki kisiki wa Simba Pascal Wawa.

BEKI kisiki wa Simba Pascal Wawa anarejea Uwanjani wiki ijayo kuwavaa Singida United, mara baaada ya kukaa nje ya Uwanja kwa muda wa mwezi mmoja akiuguza majeraha ya mguu.

 

Wawa aliumia katika mchezo wa kwanza Simba ikiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe, kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali katika uwanja wa Taifa, Dar.

 

Wawa ameeleza kuwa aliambiwa na daktari wake akae nje ya Uwanja kwa wiki mbili bila kufanya mazoezi ya aina yoyote kutokana na aina ya majeraha aliyopata.

Akizungumza na Spoti Xtra, Wawa alisema; “Natarajia kurudi Uwanjani wiki ijayo baada ya kukaa nje kwa muda wa mwezi mmoja, nafikiri hilo ni jambo linalowezekana nimeshaanza kufanya mazoezi makali chini ya kocha wa viungo Adel Zrane.”

+255 GLOBAL RADIO UCHAMBUZI WA MAGAZETI MEI 16

Comments are closed.