The House of Favourite Newspapers
gunners X

Waziri Mkuu Aagiza Uboreshaji wa Huduma za Vivuko Kigamboni

0

Dar es Salaam, Desemba 24, 2025 – Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka mamlaka zinazohusika na usafiri wa vivuko vya Kigamboni kuangalia njia za kurahisisha huduma, hasa kwa wanafunzi na wagonjwa wanaovuka kwenda upande mwingine.

Akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika kivuko cha Magogoni, Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imejipanga kuboresha usafiri wa vivuko kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wakazi wa Kigamboni wanapata huduma bora, rahisi na za haraka.

Hii inajiri huku vivuko vya Kigamboni vikikabiliwa na foleni ndefu za magari na abiria, jambo ambalo limekuwa changamoto kwa wanafunzi, wagonjwa na wananchi wengine wanaosafiri kila siku.

Leave A Reply