The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Kufungua Kongamano La Bima Ya Afya Kwa Wote

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 30, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mdahalo wa Bima ya Afya kwa Wote na Jukwaa la Kitaifa la Ugharamiaji wa Huduma za Afya kwa ajili ya utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote (Universal Health Insurance – UHI).

Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha, limelenga kuwashirikisha wadau wote muhimu kuweka mikakati madhubuti ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.

Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni “Ugharimiaji endelevu wa huduma za afya nchini: Kuimarisha mfumo wa Bima ya Afya ili kufikia afya kwa wote 2030”

 

Leave A Reply