The House of Favourite Newspapers

Wema Akesha Akimlilia Tundu Lissu

0
Wema Sepetu.

TUKIO la kushambuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida-Mashariki, Tundu Lissu ambaye ni wakili na Mwanashieria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limewaliza wengi akiwemo staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ambaye anadaiwa kukesha akilia hivyo kuibua sintofahamu kwa watu waliomzunguka.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Wema ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, taarifa hizo zilimchangaya hasa ukizingatia kuwa Lissu ni ndugu yake na pia ni wakili wake katika kesi inayomkabili ya matumizi ya madawa ya kulevya.

“Taarifa za Lissu kupigwa risasi zilimchanganya sana Wema. Tangu apate taarifa hizo amekuwa akilia sana hadi kila mtu akaogopa. Tulihisi anaweza akapoteza fahamu au akapata ugonjwa hivyo tulitaka kumpeleka hospitalini, akapumzishwe,” kilisema chanzo hicho.

Tundu Lissu.

Chanzo hicho kiliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya Wema kuangua kilio usiku kucha na mchana kutwa, mwishoni mwa wiki iliyopita alibadilisha staili ambapo alikuwa halii, badala yake aliamua kujifungia ndani akimuombea kiongozi huyo.

“Huwezi kuamini, sasa Wema amekuwa ni mtu wa kusali tu akimuomba Mungu ampe Lissu ahueni na hali yake ilirudi kama zamani,” kilisema chanzo.

Katika kutafuta ukweli wa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Wema ili kuthibisha madai hayo ambapo alisema kuwa, hakuna kitu kilichomuuma kama hicho na bado kitaendelea kumuumiza hadi aone hali ya Lissu inatengemaa na kurudi kwenye majukumu yake ikiwemo kumtetea kwenye kesi yake.

“Naendelea kuumia hadi nitakapomuona Lissu akiwa katika hali nzuri kama mwanzoni,” alisema Wema.

Stori: IMELDA MTEMA | IJUMAA WIKIENDA|DAR

Gwajima Aliamsha Dude Kushambuliwa Kwa Tundu Lissu

Leave A Reply