Wema Amnyatia Zari!

 DAR ES SALAAM : Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, ameanza kumnyatia mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kimyakimya kutokana na kuanza kupata madili makubwamakubwa ya kuweza kuyabadilisha maisha yake.

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa, anamshukuru mno Mungu kwa kusikia ombi lake baada ya kupata madili mawili ambayo yote yatamfanya azidi kusonga.

“Unajua siku zote Mungu hamtupi mja wake hata kidogo na mimi ameweza kunibariki, nimepata madili makubwa mawili na pesa yake kwa kweli siyo ndogo, naweza kufanya vitu vizuri,” alisema Wema.


Wema alisema kuwa, katika madili hayo, moja alilipata baada ya kuwa Balozi wa Star Times na lingine jipya na nono kabisa amelipata kutoka nchini Kenya.

“Huu ni wakati wa kupiga kazi sasa na ninashukuru Mungu ananisaidia mambo yangu yanaenda vizuri sana kila kupokucha na ninamuomba azidi kunisimamia,” alisema Wema.

Gazeti la Ijumaa linafahamu kuwa katika dili lake la Star Times anavuta zaidi ya shilingi milioni 30.
Kuhusu dili la Kenya, Wema hakupenda kuweka wazi kiasi cha pesa anayolipwa na kampuni moja ya huko nchini Kenya.

Stori: IMELDA MTEMA, IJUMAA

Loading...

Toa comment