Wema humtoi kwenye miguu ya kuku na vichwa

STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza kuwa kati ya vyakula anavyovipenda na vikiwekwa mezani huhisi kuchanganyikiwa ni miguu ya kuku na vichwa.

 

Akichonga na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema anapenda sana miguu ya kuku na vichwa hivyo huwa anatoa oda kabisa anapelekewa popote alipo vikiwa vimekaangwa na kuwekwa pilipili nyingi.

 

“Ukinikuta kwenye harakati zangu za kula miguu ya kuku na vichwa vyake hutaamini macho yako hata ukiweka biriani hapo siwezi kuacha miguu nikala hicho chakula, maana hii miguu na vichwa ni vyakula vya kiswahili vyenye mvuto wa kipekee,” alisema Wema


Loading...

Toa comment