BREAKING: WEMA TAYARI AMEWASILI, HUKUMU YAANZA KUSOMWA KISUTU
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa, Julai 20, 2018 inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu na wenzake wawili.
Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu tayari amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili.
Hukumu ya kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mrembo na mwigizaji Wema Sepetu imeanza kusomwa na Hakimu Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam muda huu
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL
Comments are closed.