The House of Favourite Newspapers

Wema: Yanga hii kali sana, Tukutane Taifa Leo

MIDA hii njia zote za Dar es Salaam uelekeo ni Taifa. Hata mikoa ya jirani uelekeo ni Dar Salaam tayari kuwahi Taifa kuona vifaa vya Yanga kwenye kilele cha wiki ya Mwanachi.

Yule Mlimbwende mahiri mitandaoni na kwenye jamii, Wema Sepetu nae atakuwepo Taifa tangu saa 4 asubuhi kujiandaa kuliona chama lake likikipiga na Kariobangi Sharks ya Kenya jioni. Mashabiki wote wa Yanga na wadau wa soka watashuhudia kile ambacho Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alichojigamba kwamba mziki wake msimu huu hautashikika.

Wema ambae ni Miss Tanzania 2006 ni Yanga kindakindaki na amezungumza mambo kadhaa na Spoti Xtra ambalo alilitembelea kwenye ofisi zake zilizopo Sinza Mori Jijini Dar es Salaam;

 

UMEANZA KUSHABIKIA YANGA LINI

“Nimeanza kushabikia Yanga tangia nikiwa mdogo,lakini hilo
watu hawalitambui kwa kuwa nilikuwa najihusisha na masuala ya urembo Zaidi lakini marafiki zangu wa karibu pamoja na wazazi wangu walikuwa wanatambua kuwa nashabikia Yanga.

NANI ALIYEKUSHAWISHI KUISHABIKIA YANGA

“Ni mimi mwenyewe niliipenda tu Yanga maana nakumbuka wakati naanza kukua Yanga ilikuwa ikifanya vizuri, watu wanahisi naipenda Yanga kwa kuwa labda ya wazazi wangu. “Kwanza wanatakiwa watambue baba yangu mzee Isaac Sepetu alikuwa shabiki wa Simba.

 

YANGA INAPOFUNGWA UNAKUWA KATIKA HALI GANI

“Huwa naumia kwa kuwa hakuna shabiki anayependa kufungwa, kila mtu anahitaji ushindi hivyo huwa naumia tunapofungwa haswa na Simba maana unafahamu kuwa ndio wapinzani wetu haswa, na unafahamu jinsi gani Simba walivyo na midomo wanaongea sana.

KUTOKANA NA USAJILI MLIOUFANYA MNAWEZA KUWAPOKONYA UBINGWA
SIMBA “Usajili huu ni mkubwa sana na nauamini utatusaidia sana kwani wachezaji waliosajiliwa wengi ni wazuri hivyo Simba wajiandae haswa maana hilo halina ubishi kuwa sisi ndio mabingwa wa msimu wa mwaka 2019/2020.

 

KIPI UNAJIVUNIA KWA WEWE KUWA SHABIKI WA YANGA

“Kwanza sisi ndio tunaongoza kwa kuchukua ubingwa mara nyingi hapa nchini na wapinzani wetu Simba wanaelewa hilo na mimi najivunia sana, najivunia sana na bado nitaendelea kujivunia maana nina uhakika wa kuchukua ubingwa mwingine msimu ujao, kutokana na usajili makini tulioufanya Yanga.

 

MCHEZAJI GANI ANAKUVUTIA ZAIDI YANGA

“Wachezaji wote kwangu ni bora hata hawa ambao wamesajiliwa ni bora pia, siwezi kumtaja mchezaji mmoja kuwa ananivutia zaidi kwa kuwa naipenda Yanga basi inanibidi niwapende wachezaji wote maana ndio Yanga wenyewe.

ULISHAWAHI KUFIKIRIA KUISHABIKIA SIMBA

“Hapana kwa kweli sijawahi kufikiria hilo japokuwa baba yangu Isaac Sepetu alikuwa ni shabiki wa Simba lakini sikuwahi kufikiria kuishabikia Simba, mimi nitabaki kuwa shabiki wa Yanga pekee. Kingine kinachonifanya nisiipende Simba mashabiki wao wanaongea sana, yaani wamechukua ubingwa hivi karibuni wana makelele kweli yaani ndio maana siwapendi.

YANGA IPO KATIKA WIKI YA MWANANCHI, UNAIZUNGUMZIAJE WIKI HII;

“Kwanza ni mara yetu ya kwanza kuifanya hivyo ni jambo jema kuona tumefanikiwa katika jambo la kwanza lakini bado tunazidi kujifunza kupitia hii ya kwanza ambapo nina imani tutaenda kuiboresha zaidi hapo mwakani tutakapoifanya ya pili. Lakini jambo la msingi ni mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi ili kuujaza uwanja wote na kuviona vifaa vipya vitakavyoipa ubingwa Yanga msimu ujao Cha mwisho ili wiki yetu ikamilike vizuri basi tunatakiwa kupata ushindi dhidi ya Kariobangi Sharks naamini hapo tutakuwa tumeikamilisha wiki yetu vizuri.”

Comments are closed.