The House of Favourite Newspapers

‘WEZESHA MZAWA’ YATOA ELIMU YA MIKOPO MUHIMBILI

Meneja wa Tawi la kampuni ya Wezesha Mzawa, Maimuna Tumba (aliyesimama mbele, wa tatu kulia) akiwatambulisha viongozi wa kampuni yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Shamim Mshana.
Baadhi ya wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (MOI) wakimsikiliza Tumba (aliyesimama kulia) katika hafla hiyo.
Wauguzi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.

 

Mhamashishaji maarufu nchini kuhusu ujasiriamali, Eric Shigongo (aliyesimama kushoto) alihudhuria hafla hiyo na kuwatia moyo washiriki kwa kuwahimiza kujiongezea vipato baada ya kazi na kuitumia kampuni ya Wezesha Mzawa ili kupata mitaji ya kujikomboa kiuchumi.
Meneja Mkuu wa Wezesha Mzawa Microfinance, Shamimu Mshana, akifafanua jambo katika hafla hiyo.

      

KAMPUNI inayotoa ya Mikopo Wezesha Mzawa Microfinance Ltd leo imetoa elimu kuhusu huduma zake za mikopo yenye riba nafuu na haraka.

 

Elimu hiyo ilitolewa leo kwa wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (MOI) jijijni Dar es Salaam ambapo meneja wa Tawi la kampuni hiyo, Maimuna Tumba, amesema kuwa kampuni yao inatoa fursa kwa Watanzania binafsi ikiwa ni pamoja na kulipia ada za masomo kwa watoto na wanafunzi.

 

Alifafanua kwamba mikopo ya kampuni hiyo huchukua muda mfupi zaidi kutolewa kwa ajili ya kulipia ada za ngazi zote kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kwa riba na masharti nafuu ambayo mkopaji anatakiwa kuwa Mtanzania mwenye umri usiokuwa chini ya miaka 18.

 

Aliongeza kwamba mkopaji anaweza kuwa mfanyakazi au mfanyabiashara ambaye atawajibika kuleta vielelezo vya shule au chuo husika ili ofisi iweze kuvihakiki na akikidhi vigezo fedha hutalipwa moja kwa moja kwenye shule au taasisi husika.

 

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Wezesha Mzawa Microfinance, Shamimu Mshana, alifafanua kuwa lengo hasa ni kutoa suluhisho la kweli kwa watu wenye mahitaji ya fedha kwa uharaka na muda mfupi.

 

“Tunatoa kwa mfanyabiashara halali anayezingatia ulipaji kodi katika mamlaka husika na mkopaji anaweza kurudisha kiasi alichokopa kulingana na yeye mwenyewe atakavyoona kwa mujibu wa mahitaji yake, ” alisema.

 

Naye, mhamasishaji mashuhuri wa ujasiriamali nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa Wezesha Mzawa Microfinance aliyehudhuria hafla hiyo, Eric Shigongo, aliyefika hapo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwapa mbinu za kujikwamua kiuchumi washiriki, alisema kuwa haiwezekani mfanyakazi akawa anasubiri mshahara tu na kwamba ni lazima atengeneze vitegauchumi vingine ili aondokane na umaskini.

 

Amesema wafanyakazi wengi hutumia kigezo cha kwamba muda wa kutoka kazini ni mrefu na hivyo wanashindwa kufanya majukumu mengine ya kujiongezea kipato.

 

Pamoja na hivyo, aliwashauri kuondokana na dhana hiyo na wautumie muda huo wa kuanzia jioni kwa kufanya kazi za kuwaongezea vipato kiuchumi.

 

Aliwashauri waitumie kampuni hiyo ya Wezesha Mzawa Microfinance Ltd ili waongeze mitaji yao na kuendeleza biashara

Comments are closed.