The House of Favourite Newspapers

YANGA ‘KUBWA KULIKO’: JK AFUNGUKA ALIVYOWAPA UWANJA SIMBA

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,  amesema viongozi wa serikali hawatakiwi kuegemea katika klabu moja na kukandamiza nyingine kwa sababu zote ni za Watanzania na wao ni viongozi wa Tanzania huku akitolea mfano kuwa yeye akiwa rais aliwahi kuwapa Simba pesa kiasi cha Tsh milioni 30 kwa ajili ya kununua eneo la kujenga uwanja wao wa mazoezi.

 

Kikwete amesema hayo leo Jumamosi, Juni 15, 2019,  wakati akitoa neno kwenye hafla ya uzinduzi wa harambee ya kuichangia Yanga iliyofanyika katika Ukumbi nwa Diamond jubilee, jijini Dar es Salaam.

 

“Kuna wakati Prof. Sarungi na Juma Kapuya walikuwa mawaziri wa michezo na hawa wote ni Simba kindakindaki lakini hawakutumia nafasi zao kuikandamiza Yanga. Nilipokuwa rais Simba walitaka kununua kiwanja kule mabwepande lakini hela hawana, Aden Rage alikuja kwangu kuniambia wanahitaji milioni 30 kwa ajili ya kiwanja nikawaambia hizo mmepata.

 

“Nayasema haya kwa uwajibu wa uongozi.. kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu, Yanga wana shughuli na wewe utoe, sikumbushii kama deni ila nawaombea Wanayanga wenzangu mchango ukamuambie na Mheshimiwa Rais na yeye atoe.

“Mimi nimeshiriki sana shughuli za Yanga si kidogo tena mara nyingi. Nakumbuka usajili wa marehemu Sikinde kutoka Majimaji kuja Yanga jinsi ulivyokuwa hadi tukamleta Yanga. Sasa Yanga mna uongozi nawapongeza sana mliochaguliwa embu nendeni kabadilisheni hii hali, Yanga ni klabu ya wanachama kuna wakati mlitaka kunisononesha kuibadilisha iwe timu ya mtu mmoja hapana hii si sawa.

 

“Nawategemea Msolla na wenzako timu nzuri sana uzuri mmechaguliwa watu mnaojua mpira maana kuna watu wanachaguliwa kwa ajili ya umaarufu wao. Ukiona yupo kiongozi mmefungwa amelala mkishindwa sawa,  huyo si kiongozi wa Yanga.

 

“Msolla na wenzako leteni usasa kwenye soka letu na uendeshaji wenye tija na wekezeni kwenye soka la watoto kama alivyofanya Kocha Victor Stanslaus kwa matunda ya Sunday Manara, Mohamed Mkweche, Kassim Manara na wengine hawa kizazi cha watoto cha Yanga.

 

“Mnawekeza kwenye soka kwa wachezaji wa nje na makocha wa kigeni hii si faida ya taifa,  mnaona fahari kwa wachezaji wa nje. Waendelezeni vijana wetu sisi zamani, alisisitiza na kuongeza:

 

“Wewe Msolla kama mwenyekiti tengeneza timu ya watoto wakati hata wa ‘Part Time’ (muda wa ziada) wafundishe huku Mwinyi Zahera akifundisha timu ya wakubwa lakini pia tengenezeni mapato endelevu ya timu yetu.”

 

 

Comments are closed.