The House of Favourite Newspapers

Yanga Kuja na Surprise kubwa kwa mashabiki na wanachama leo

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa utakuja na Surprise kubwa kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwenye mkutano mkuu wa mwaka.

Juni 9 2024 Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wanatarajia kufanya mkutano katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watafanya mazuri kwa mpangilio mkubwa ikiwa ni pamoja na surprise kubwa kwa wananchi.

“Mpango upo sawa na maandalizi kwa asilimia kubwa yapo vizuri ni suala la muda tu. Wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwani tunakuja na Big Surprise kwa ajili yao.

“Msimu ulikuwa na mengi tumeona namna ushindani ulivyokuwa na pale ambapo tupo kwa sasa ni muhimu kutazama yale yajayo kwani kuna mengi mazuri yanakuja.”

Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 wakiwa na pointi 80 baada ya mechi 30 watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Stori na Luyamadzo Mlyuka, Championi, GPL

KATIBU MKUU ENZI za NYERERE ATAPELIWA KIWANJA na MUSHI – WAZIRI SILAA AINGILIA na KUMREJESHEA…