YANGA KUKIPIGA NA TANZANIA PRISONS BILA GADIEL LEO

YANGA leo Alhamisi wanapambana na Tanzania Prisons ambapo beki wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael anaweza asiwepo kwenye mechi hiyo baada ya kupewa mapumziko ya siku tano nje kutokana na majeraha ya enka aliyoumia Jumatatu hii akipambana na Azam FC.

 

Gadiel Jumatatu hii aliondolewa uwanjani na gari la msaada kwa wagonjwa (ambulance) na kukimbizwa Hospitali ya Temeke baada ya kupata majeraha ya enka kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Azam FC, ambayo Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

 

Daktari wa Yanga, Edward Bavu ameliambia Spoti Xtra, kuwa baada ya kumfanyia vipimo beki huyo ikiwemo X-ray wamempa muda wa kupumzika kwa siku tano kabla ya kurejea tena kuanza kuichezea klabu hiyo huku akikosa mechi ya leo Alhamisi dhidi ya Prisons.

“Gadiel baada ya kuondolewa pale uwanjani alipelekwa Hospitali ya Temeke ambapo alienda kufanyiwa vipimo ikiwemo kupigwa x-ray ili kuangalia ukubwa gani wa jeraha lake.

 

“Lakini baada ya kuona siyo tatizo kubwa kwa kiwango hicho, tumempa mapumziko ya siku tano ambazo tunaamini zinaweza kuwa msaada kurejea vizuri na kuanza tena kucheza,” alisema Bavu. Katika mechi hiyo Gadiel alishindwa kupelekwa kwa wakati hospitalini baada ya kupata majeraha hayo kutokana na kutokuwepo kwa ambulance.

Na:SAID ALLY,


Loading...

Toa comment