Yanga SC Yampa Mkataba Kiungo Fundi

YANGA imeanza mazungumzo ya kumnunua kiungo mshambuliaji fundi mwenye mkataba na Mtibwa, Salum Kihimbwa. Kihimbwa ni kati ya viungo waliowahi kutajwa kuwaniwa na Simba, Yanga kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara kabla ya kushindwana na timu hizo kongwe.

 

Yanga hadi sasa tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wawili wazawa ambao ni kiungo mkabaji wa Mafunzo FC ya Zanzibar, Abdul Aziz Makame na kipa wa Azam FC aliyekuwa kwa mkopo Mbao FC, Mechata Mnata.

 

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra imejiridhisha nazo ni kwamba, uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na mabosi wa Mtibwa Sugar kwa ajili ya ishu ya Kihimbwa mwenye mkataba wa mwaka mmoja Manungu.

 

Habari zinasema kwamba kiungo alitarajiwa kukutana na viongozi wa Yanga juzi Jumatatu lakini matatizo ya kifamilia yalisababisha ashindwe kuonana nao huku wakipanga siku ya kuonana ili wakamilishe dili hilo.

 

Yanga wanataka kumsajili Kihimbwa kuiongezea nguvu safu ya kiungo tayari kwa michuano ya kimataifa ambayo inaanza mwezi Agosti.

 

Alipoulizwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo alisema, kama ni kweli itabainika baadae huku akisisitiza kwamba kuna watu maalum wanafanyia kazi ripoti ya kocha.


Loading...

Toa comment