The House of Favourite Newspapers

yanga, singida B. stars dimbani leo

0

Klabu ya soka ya Yanga itashuka dimbani Leo majira ya saa 2:30 usiku kukabiliana na Singida black stars, katika muendelezo wa ligi kuu ya soka ya NBC Premier League, kwenye uwanja wa Aman Zanzibar.

Yanga wenye alama 21 wakiwa nafasi ya pili, watakaribishwa na vinara wa ligi Singida black stars wenye alama 22, huku Singida blackstars wakiwa wametoka kupata ushindi wa 2-0 katika mchezo wao wa mwisho dhidi Singida Fountain Gate, wakati mabingwa watetezi Yanga waliibuka na ushindi wa 0-1 dhidi ya Coastal union kule Arusha.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Singida blackstars alitamba kuwa Yanga watakutana na timu ambayo haijapoteza mchezo mpaka Sasa, wakati kocha Miguel Gamondi akilalamikia ratiba Kwa kusema kuwa ”tumecheza mechi 7 ndani ya siku 21 sio jambo jepesi kujiandaa katika mazingira kama haya”.

Mpaka sasa Yanga wamecheza michezo 7, wakati Singida black stars wamecheza michezo 8, tofauti yao ikiwa ni alama moja tu hivyo kama Yanga atashinda atapanda mpaka juu kwenye msimamo huo na endapo Singida black stars atashinda atazidi kujikita kileleni katika msimamo huo.

Leave A Reply