The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tutarudi Tukiwa Imara, Ally Kamwe Afunguka Mazito

0

BAADA ya kufungashiwa virago kwenye Kombe la Mapinduzi 2024, uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa utarejea kwa wakati mwingine ukiwa imara kwa kupambania malengo ya kutwaa taji hilo.

Ipo wazi kuwa Yanga kwenye mechi nne ilizocheza ilishinda mechi mbili, sare moja na ikipoteza mchezo mmoja katika hatua ya robo fainali.

Mchezo huo wa kwanza kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kupoteza kwa 2024 ilikuwa Januri 7 ubao wa Uwanja wa Amaan uliposoma Yanga 1-3 APR FC.

Ally Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga amesema walikuwa kwenye mwendo mzuri awali na kupoteza mchezo ni sehemu ya matokeo hivyo wanajipanga kwa wakati ujao.

“Kwa kilichotokea tunashukuru kwa kuwa kila mmoja ameona namna ambavyo wachezaji walikuwa wakipambana mbele ya mpinzani aliyepata matokeo hivyo tunashukuru kwa yote na kuwaambia mashabiki kwamba tutarejea wakati ujao tukiwa imara.

“Mapinduzi 2024 kwetu safari yetu imefika mwisho ni muda wa kuanza kutazama mengine yanayokuja. Wakati ujao tukirudi tunaamini tutakuwa kwenye ubora zaidi na tutapambana kufikia malengo ya kutwaa taji la Mapinduzi,”.

Leave A Reply