The House of Favourite Newspapers

FT: YANGA Vs SIMBA LIVE UWANJA WA TAIFA, NGAO YA JAMII

Mashabiki wa Simba.

 

FULL TIME

Simba imepata ushindi wa penati 5-4 baada ya matokeo ya 0-0. Waliokosa penati upande wa Yanga ni Kelvin Yondani na Juma Mahadhi, aliyekosa wa Simba ni Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, SASA NI MKWAJU YA PENALTI
Dk 90+2 Niyonzima anamchambua Gadiel, anaachia mkwaju mkali kabisa lakini juuuuuuuu
Dk 90+2 Gadiel anafanya kazi ya ziada, anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Yanga wanaokoa

Kelvin Yondani akicuana vilivyo na Okwi.

 

Dk 90+1, Simba wanapata kona hapa, inachongwa na Kichuya lakini mpira unakwenda nje, goal kick

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Simba wanaendelea kumiliki mpira lakini hawana malengo yanayotimia langni mwa Yanga ambao wako makini kiulinzi
SUB Dk 88, Mohamed Zimbwe Jr, anaingia kuchukua nafasi ya Nyoni ambaye ameumia
Dk 88 sasa, Nyoni yuko chini pale anatibiwa, mchezo umesimama

SUB Dk 87, Yanga wanamuiginza Hassan Kessy anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul
KADI Dk 87 Yondani analambwa kadi ya njano hapa
Dk 85 sasa, Simba ndiyo wamemiliki mpira kwa muda mrefu zaidi lakini wajanja kuipita ngome ya Yanga

Tshimbi na Yondani.

Dk 81, Mo Ibrahim, lakini kipa wa Yanga anafanya kazi kubwa kuokoa mpira huo, anamgonga Vicent, yuko chini anatibiwa
Dk 80, Simba wanapata kona, inachongwa, Kichuya anajaribu lakini Yanga wanaokoa
Dk 79 Martin anaingia na kuachia mkwaju mkali, Manula anaokoa lakini mwamuzi anasema ilikuwa faulo
SUB Dk 78 Mohamed Ibrahim anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru

Ngoma nzito.

 

Dk 77 Tshishimbi ameachia shuti kali hapa lakini hakulenga lango
Dk 76, umbali wa takribani mita 25 lakini hakulenga lango
Dk 75, Gadiel anatoka katika nafasi yake, anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira miguuni kwa Liuzio ambaye kama angepiga, yangekuwa mengine
SUB Dk 73 Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Raphael Daud
SUB Dk 72 Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo upande wa Simba
Dk 72, Martin anaachia krosi safi kabisa langoni mwa Simba, lakini hakuna mtu
Dk 69 sasa, mpira umebaki katikati mrefu na inaonekana kutakuwa na shambulizi la kushitukiza upande mmoja litakalozua madhara

Niyonzima akijaribu kumtoka Kamusoko.

 

Dk 65, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, mabeki wa Simba wamezidiwa ujanja, lakini Manula anatoka na kuokoa
Dk 62, Ajibu anamfanyia madhambi Shomari, mwamuzi anampa onyo kwa mdomo tu akimsisitiza kutulia
Dk 60, mechi bado inaonekana haina spidi kali kama ambavyo ilitarajiwa. Lakini Yanga wanaonekana kuna kitu wanatafuta na hasa kwa shambulizi la kushitukiza kwa kuwa wanajaza wachezaji wengi nyuma kwa ulinzi na Simba wanaonekana kujisahau mara kadhaa
Dk 56, Okwi anamzidi kasi Yondani, anabaki yeye na kipa lakini Kipa Mcameroon anafanya kazi nzuri kabisa, anaokoa miguuni mwa Okwi.

 

Dk 53, Kamusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini unapita juu ya lango  Simba, angelenga ingekuwa hatariiii
KADI DK 50, Kadi ya tatu ya mchezo, Niyonzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Juma Abdul aliyempokonya mpira
Dk 48, krosi fupi ya Nyoni, Mavugo anaruka peke yake na kupiga kichwa safi lakini Goal Kick
Dk 47, Okwi anaachia mkwaju mkali hapa lakini gadiel anaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa
DK 46, Juma anamimina krosi safi kabisa lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 45, Mechi imeanza na Simba wanafanya shambulizi kali, Okwi anaingia lakini Youthe anaokoa vizuri kabisa hapa
MAPUMZIKO


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44 sasa, mpira unachezwa katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makali
Dk 41, Simba wanajibu shambulizi na kupata konaaaa, inachongwa na Kichuya na Niyonzima anaachia mkwaju mkali sana, goal kick
Dk 41, Yanga wanafanya shambulizi lakini Manula anatoka na kuuwahi mpira

Dk 40, krosi nzuri ya Nyoni, Mavugo anashindwa kulenga hapa
KADI Dk 38, kadi ya pili ya mchezo wa leo, inakwenda kwa Juma Abdul baada ya kumuangusha Kotei
Dk 35, pasi nzuri ya Niyonzima, Mavugo anapiga krosi, Yondani anapiga kichwa na kuwa kona, Yanga wanaokoa vizuri kabisa
Dk 33, Mavugo anageuka vizuri na kuachia mkwaju mkali hapa lakini Yondani anafanya kazi ya ziada
Dk 32, Simba wanapata kona ya kwanza baada ya kufanya shambulizi, inachongwa hapa na Niyonzima lakini Yanga wanaokoa vizuri hapa
KADI Dk 31 kadi ya kwanza ya njano inatoka, MWanjale anafanya upuuzi kwa kupiga mpira chini kwa nguvu wakati filimbi ilishapulizwa.

Dk 29 sasa, kidogo presha ya mchezo imehamia tena katikati kila timu ikionekana kutulia na kutaka kujipanga
Dk 27, Yondani anamdhibiti Mavugo hapa, analazimika kufanya faulo, inapigwa kwenda Simba

Dk 24, Martin anaachia mkwaju mkali hapa akipokea pasi ya Kamusoko, lakini hakulenga lango
Dk 23 Kipa Rostand, anafanya kazi nzuri kwa kudaka mpira wa juu wa krosi wa Nyoni
Dk 22, Ngoma anaingia vizuri kabisa lakini Mwanjale anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 22 sasa, Yanga wanaonekana kujilinda zaidi huku Simba wakiwa wameshambulia zaidi lakini ukiangalia difensi ya Simba inaonekana kuachia nafasi ambazo Yanga wakiwa makini wanaweza kuzitumia hasa kwa pasi za kupitisha
Dk 20, Okwi anaingia tena, anaachia mkwaju hapa lakini Yondani anaiokoa vizuri kabisa

Dk 18, Niyonzima aanaingia na kuchambua vizuri, lakini basi aliyompa Muzamiru anapaisha buuuuu.

Dk 16, Simba wanatangeneza nafasi nzuri zaidi, krosi ya Nyoni, Dante anaonekana kuzubaa na Mavugo anapiga kichwa lakini hakulenga
Dk 15 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna shambulizi kali

Dk 10, Niyonzima anachambua msitu, lakini Ngoma anasema hapana anamuweka chini hapa, faulo
Dk 9, Manula anamuwahi Ngoma na kuutoa mpira nje unakuwa wa kurusha

Dakika ya 9: Simba wanakuwa wazito kufanya maamuzi, Yanga wanafika langoni mara kadhaa.

Dakika ya 8: Yanga wanamiliki mpira na kutengeneza njia za kufunga lakini wanashindwa kutumia nafasi.

Dakika ya 6: Simba wanafika langoni mwa Yanga.

Dakika ya 5: Yanga wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

Dakika ya 4: Ibrahimu Ajibu anachezewa faulo na beki wa Simba, Mbonde nje ya eneo la 18 wakati akielekea golini. Inakuwa faulo/

Dakika ya 2: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, wanapiga pasi nyingi eneo lao.

Shangwe ni nyingi kutoka pande zote, idadi ya mashabiki ni kubwa.

DK 1: Mchezo umeanza.

 

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, wapo uwanjani kukipiga dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA katika mchezo wa Ngao ya Jami kuukaribisha msimu wa 2017/18.

Kikosi cha Simba kinachoanza leo

1. Aishi Manula

2. Ally Shomari

3. Erasto Nyoni

4. Salim Mbonde

5. Method Mwanjale

6. James Kotei

7. Shiza Kichuya

8. Mzamiru Yassin

9. Laudit Mavugo

10. Emanuel Okwi

11. Haruna Niyonzima

WALIOPO BENCHI

1. E. Mseja

2. M. Tshabalala

3. Juuko M

4. J. Mkude

5. M.Kazimoto

6. J Luizio

7.MO Ibrahim

Kikosi cha Yanga

1.Rostand Youthe

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Andrew Vicent

5. Kelvin Yondani

6. Papy Tshishimbi

7. Raphael Daud

7. Thaban Kamusoko

9. Ibrahim Ajibu

10. Donald Ngoma

11. Emmanuel Martin

WALIOPO BENCHI

Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Haji Abdallah, Mwinyi Haji, Juma Makapu, Yusuph Mhilu, Juma Mahadhi.

Comments are closed.