Young Dee, Young Killer Uso kwa Uso Idd El Fitr Dar Live

David Genzi ‘Young Dee’

WAKALI wawili wasioshikika kunako gemu ya Muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’ pamoja na David Genzi ‘Young Dee’ wanatarajiwa kukutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza Sikukuu ya Idd el Fitr ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Star Showbiz, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, kwa muda mrefu mashabiki walikuwa na kiu ya kuwaona Young Dee na Young Killer wakipimana uwezo jukwaani hivyo Dar Live imeona itakuwa jambo la kheri kama ‘wakimalizana’ jukwaani katika shoo iliyopewa Usiku wa Nani Atazima.

 

“Hakuna asiyefahamu kama Young Dee na Young Killer ni wasanii wakali ambao mara kwa mara kila mmoja amekuwa akijiona yupo juu ya mwenzake. Baada ya kushindana nje ya jukwaa kwa muda mrefu Dar Live tumewaletea moja kwa moja ambapo Sikukuu ya Idd unavyofikiria wewe nani atazima mbele ya mwenzake?” Alisema KP. Ngoma zao sasa!

 

 

KP aliongeza kuwa, usiku huo utakuwa wa bandika bandua ambapo kila mmoja atahakikisha anaondoka na kijiji.

“Young Killer anazo ngoma kibao ambazo zitawasimamisha mashabiki wengi, ngoma kama vile Kumi na tatu (13), True Boya, Hujanileta, Popote Kambi, How we Do, Dear Gambe, Jana na Leo, Umebadilika, Mrs Superstar na nyingine kibao.

 

“Upande wa Young Dee naye anazo ngoma kibao kama vile Hands Up, Bongo Bahati Mbaya, Kiben10, Tunapeta, Kiutaniutani, Tunapeta na nyingine nyingi,” alisema KP. Wakali wengine wapo Mbali na uwepo wa Young Killer na Young Dee, KP alisema k Live pia itafunikwa na wakali wa Singeli Msagasumu na Man Fongo.

 

“Pata picha ukimsikia Msaga Sumu na Ngoma ya Unanitega Shemeji huku upande wa pili msikie Man Fongo na Ngoma ya Hainaga Ushemeji, yaani usiku huo ni kushuhudia nani atazima,” alisema KP.

Burudani kwa watoto Shoo ya mapema itakuwepo mapema kuanzia asubuhi kwa burudani kabambe ya watoto.

“Tutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kuogelea, kucheza na baiskeli spesho, kuvutana kamba kupanda ndege spesho pamoja na kuogelea huku burudani ya sarakasi na kucheza muziki ikitolewa na Wakali Dancers,” alimaliza KP.

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment