The House of Favourite Newspapers

Zahera Amkataa Djuma Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa mkataba wake unampa ruhusa ya kufanya kazi na kocha yeyote anayemtaka yeye, akiwemo Masoud Djuma lakini hawezi kufanya hivyo kwa kuwa waliopo ni wazuri zaidi kwake.

Zahera, mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, ameyasema hayo baada ya Simba kuachana na kocha wake msaidizi, Masoud Djuma raia wa Burundi kufuatia madai ya kutoelewana na kocha mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera alisema kuwa hawezi kukubali kufanya kazi kwa sasa na kocha yeyote bila idhini yake, kwa kuwa tayari ana mtu makini anayeifanya vizuri kazi yake kwenye kikosi cha timu hiyo.

 

“Nasikia Djuma anakuja Yanga ila kama amefukuzwa Simba, mimi sifahamu hayo mambo na sitaki mtu mwingine kwa sababu uongozi unajua wakati wanasaini mkataba iliandikwa Kocha Mwinyi Zahera ni yeye peke yake anaweza kuchagua watu wake wa benchi la ufundi anaowapenda kufanya nao kazi.

“Binafsi sioni ulazima wa kutafuta kocha mwingine kwa sababu yupo msaidizi wangu, Noel Mwandila, ni kocha mzuri na anajua kazi vizuri sasa, kuna haja gani ya kumchukua huyo anayesemwa?” alihoji Zahera.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam.

“Nyerere Anafanana na JPM” – NABII NYAKIA

Comments are closed.