The House of Favourite Newspapers

Zahera Amlipia Akilimali Sh 369,000 Muhimbili

Ibrahim Akilimali

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemlipia Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, kiasi cha shilingi za Kitanzania 369,000 alizokuwa anadaiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 

Zahera amemlipia Akilimali fedha hizo zilizotokana na kufanyiwa matibabu katika hospitali hiyo baada ya kuomba msaada kwa wadau mbalimbali ili wamchangie.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Akilimali amesema Zahera ameamua kumsaidia baada ya kupata taarifa zake kupitia Gazeti la Spoti Xtra ambalo hutoka kila Alhamisi na Jumapili na linachapishwa na Global Group.

Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Akilimali ameeleza kuwa Zahera aliguswa alipoona taarifa hiyo na kuamua kujitoa kumlipia fedha zote hizo huku akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Global Group kwa mchango wake kwake.

 

“Ni kweli Zahera amenilipia deni lote ambalo ni Sh 369,000 na nimeshalipa tayari, sidaiwi tena.

“Aliona taarifa kupitia gazeti lenu la Spoti Xtra na akaguswa hivyo akaamua kunisaidia, kwa kweli nawashukuru sana Global kwa mchango wenu, mmenisaidia.

 

“Siwezi kuwa mchoyo wa fadhila kumshukuru sana Zahera, ameonesha ni mtu wa watu ukiachana na masuala ya mpira, pia shukrani kwa baadhi ya wadau wengine waliojitoa kunichangia,” alisema Akilimali.

 

Akilimali amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu ambao umekuwa ukisababisha hali yake kiafya kutokuwa nzuri.

 

Ikumbukwe kabla ya Zahera kumlipia deni hilo, mpaka kufikia Jumatano ya wiki iliyopita Akilimali alikuwa ameshapokea zaidi ya shilingi 34,000 ambazo alikuwa akitumiwa na wadau walioguswa na tatizo lake.

Stori: George Mganga, TUDARCo

UCHAMBUZI: NAPE AMERUDI ANALIA kwa MAGUFULI | GLOBAL RADIO

Comments are closed.