Zahera aweka hadharani mastaa 8

YANGA ikimaliza mechi na Azam tu kwenye Uwanja wa Uhuru Jumanne ijayo, Kocha Mwinyi Zahera ataweka hadharani mastaa wote wapya nane kabla ya kutimkia Hispania.

 

Kauli hiyo, aliitoa jana wakati timu hiyo ikiwa inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kumsajili mbadala wa mshambuliaji wake Mkongomani, Heritier Makambo aliyesaini tayari mkataba wa awali Horoya AC ya nchini Guinea.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema Mei 28, mwaka huu mara baada ya mchezo dhidi ya Azam atasafiri kwenda Hispania kwa ajili ya kujiunga na kambi ya pamoja ya DR Congo inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa Afrika zitakazofanyika nchini Misri.

 

Zahera alisema kuwa, anataka kabla ya kusafiri awe tayari ameshakamilisha usajili wa wachezaji kwenye baadhi ya nafasi ikiwemo ya ushambiliaji kwa kumleta mshambuliaji mwingine zaidi ya Makambo.

 

Aliongeza kuwa, kati ya washambuliaji hao yupo mmoja kutoka Gabon raia wa DR Congo aliyemalizana naye huku akisubiri fedha tu ili atue nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuichezea Yanga.

 

“Tukiwa tunajiandaa kumalizia ligi, tunaendelea na matayarisho ya timu yetu kwa kusajili wachezaji wenye ubora watakaoipa mafanikio Yanga katika msimu ujao

 

“Nafahamu mashabiki wa Yanga baadhi wanaumia kuondoka kwa Makambo lakini niwaambie kuwa, ninao washambuliaji wengi watakaokuja msimu ujao na kufanya vizuri zaidi yake.

 

“Kwa kuwaondoa hofu mashabiki wa Yanga kuwa kabla ya mimi kuondoka nchini kwenda Hispania itakapokwenda kuweka kambi Timu ya Taifa ya DR Congo Mei 29, mwaka huu ninataka niwe nishasaini wachezaji nane ambao nitawatambulisha kabla ya kuondoka na kati yao atakuwepo mbadala wa Makambo.


Loading...

Toa comment