The House of Favourite Newspapers

Zidane Ataka Dili la Pogba Fasta

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameupa uongozi wa Real Madrid mtihani mzito baada ya kuwataka kuhakikisha wanamsajili Paul Pogba.

 

Uongozi wa Real Madrid unagwaya bado kuonana na Manchester United kutokana na ukweli kuwa mkataba wake unamalizika mwaka 2021.

 

Hata hivyo, Zidane anamtaka staa huyo, ambaye ni Mfaransa mwenzake kwani ni miongoni mwa mastaa anaowahitaji sana kuwapata. Pogba mwenyewe anataka kujiunga na Real Madrid kutokana na kuchoshwa na mwenendo wa hali ya mambo katika klabu ya Manchester United.

 

Hata hivyo, Pogba amewarahisishia kazi Real Madrid kwa kitendo chake cha kugomea kuongeza mkataba wa kuchezea Manchester United.

 

Suala lake bado ni gumu kwa kuwa uongozi wa Manchester United unataka kubaki na Pogba kutokana na manufaa yake ndani ya nje ya uwanja.

 

Pogba ni miongoni mwa mastaa wanaoongoza kwa kuuza jezi nyingi katika klabu hiyo. Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa Manchester United itataka dau zito ili kumwachia Pogba.

 

ALI KIBA “NILIKUA Natamani ABDU KIBA Afunge MZUKA”

Comments are closed.