The House of Favourite Newspapers

Majwega: Azam FC niacheni jamani

Na Wilbert Molandi,

Dar es Salaam

KIUNGO mshambuliaji Brian Majwega ameipigia magoti Azam FC, kwa kusema inatosha kwa mateso inayompa na badala yake imruhusu ajiunge na Simba acheze kwa uhuru.

Majwega, raia wa Uganda, tayari ameanza mazoezi na Simba wiki iliyopita chini ya Kocha Dylan Kerr huku akisubiria utatuzi wa sakata lake la mkataba na Azam lililopo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Wakati Majegwa aking’ang’ania kuichezea Simba, Azam imedai bado mchezaji huyo ni wao kwani ana mkataba hai unaotarajia kuisha mwakani.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Majwega alisema kuwa haoni sababu Azam kumng’ang’ania na kudai ni mali yao wakati kisheria mkataba wake umevunjwa kutokana na kutolipwa mshahara kwa muda wa miezi sita.

Majwega alisema: “Sifikirii kurejea Azam tena kwa kuwa mapenzi yangu sasa yapo Simba, klabu ambayo naamini itanirejesha katika kiwango changu.

“Nawaomba Azam waniache huru huku nilipo nikiendelea kuichezea Simba, nilijua hao lengo lao lilikuwa ni kuniharibia kwa kutaka kunipeleka kwa mkopo KCCA.”

Comments are closed.