The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Bilioni 4 za uhuru zijenge barabara ya Mwenge – Morocco

Mwenge-Morocco (2)Barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, leo ameamuru fedha kiasi cha shilingi bilioni 4 zilizokuwa zimetengwa kama bajeti ya sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika Desemba 9, 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

Comments are closed.