The House of Favourite Newspapers

Rose Muhando ang’atwa na nyoka

8

rose_muhandoStaa anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando.

GLADNESS MALLYA Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM! MAJARIBU! Staa anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando yupo hoi kitandani baada ya kung’atwa na nyoka.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Rose akiwa anaingia getini usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwake mkoani Dodoma aling’atwa na nyoka mguuni na kukimbizwa hospitali iliyopo Area C mkoani humo.

“Maskini Rose ana majanga sana kwa kweli maana alikuwa bado hajapona ule ugonjwa wa kuvimba miguu na mikono lakini amejikuta katika wakati mgumu tena baada ya kung’atwa na nyoka nyumbani kwake,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzipata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi ambapo ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni ndugu yake, akasema;

“Hii simu imeachwa hapa nyumbani kwani dada (Rose) amepelekwa hospitali Area C, ameng’atwa na nyoka usiku akiwa anaingia getini hapa nyumbani hivyo amepumzishwa hospitali kupewa huduma ya kwanza maana ameng’atwa sana mguu na nyoka alikuwa mkubwa sana.”

8 Comments
  1. THOMAS STEPHANO says

    Nahitaji kujua ukweli wa afya ya mtumishi wa MUNGU Rose Mhando.Maana nimesikia kakumbwa na balaa akiingia kwake.

  2. Kimwama says

    LABDA LAANA YA UAVYAJI MIMBA.
    HUYU SI MTUMISHI WA MUNGU BALI WANAOTUMIA JINA LA MUNGU KUTAFUTA UTAJIRI.

  3. Amos says

    very true watu wengi hasa waimbaji wanatumia jina la Mwenyesi Mungu Kwan kutafuta utajiri.

  4. […] a snake in her compound on Tuesday last week, 19th January 2016.  Reports by Global Publisher claim that the award winning star has been suffering from another condition causing swellings on her […]

  5. shem angano says

    The best musician, ifeel sick without enjoying her songs

  6. kamau cyrus says

    behold the hand of God is not too short to safe!Let all pray 4 easy recovery for her!!!Mawazo ya mungu hayafanani na ya mwanadamu……….

  7. kamau cyrus says

    Mungu amponye

  8. annie says

    UBINAADAMU KWANZA, MENGINEYO TUMWACHIE MUNGU. MUNGU AMPONYE.

Leave A Reply