The House of Favourite Newspapers

Simba: Mkimkaba Kiiza, anawafunga Ajib

0

Ibrahim-AjibIbrahim Ajib

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
LEO Simba inacheza na Stand United katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga lakini kocha wa timu hiyo, Jackson Mayanja kuna kitu ametamka.

Mayanja ametuma salamu kwa timu pinzani katika Ligi Kuu Bara ikiwemo Yanga kwamba, hata kama zitamkaba Hamis Kiiza yupo Ibrahim Ajib ambaye atawafunga.
Kauli hiyo ameitoa Mayanja zikiwa zimebaki siku saba kabla ya timu yake kucheza na Yanga katika ligi kuu Februari 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

HAMISI-KIIZA.jpgHamis Kiiza

Mayanja alisema Kiiza ambaye ni raia wa Uganda kama ilivyo kwake, amekuwa akikamiwa na mabeki na viungo wa timu pinzani kila anaposhuka uwanjani kiasi cha kushindwa kuendelea kufunga.
Hadi sasa Kiiza ana mabao 14 katika ligi, sawa na Amissi Tambwe wa Yanga. Mayanja ameliambia Championi Jumamosi: “Najua wanamkamia Kiiza, sasa natengeneza kombinesheni tofauti za ushambuliaji ili kuepuka utegemezi wa mchezaji mmoja.
“Naona Kiiza anakamiwa sana, sasa namtengeneza Ajib naye awe anafunga kama Kiiza, najua timu zinajipanga kumzuia (Kiiza) lakini huwa zinamsahau Ajib, sasa wakimzuia Kiiza tu Ajib anawafunga.”
Mayanja alisema katika timu yake amejenga imani kwa wachezaji wake wote ambao anaamini kila mmoja na uwezo mkubwa wa kucheza uwanjani.
Simba leo inacheza na Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga katika muendelezo wa ligi kuu.

Leave A Reply