The House of Favourite Newspapers

Siyo Magufuli tu, kila mtu awe mlinzi wa mali za umma

160377-004-ECB7BCBDMwalimu Julius Nyerere.

MUNGU hapendelei ndiyo maana wote katuumba tuishi kwa kuvuta hewa ileile, miili yetu wanadamu wote ni sawa, mifupa na grupu za damu zetu ni sawa, awe Mzungu, Mwarabu, Mhindi, Mwafrika, au chotara, hivyo tumhimidi daima.

Baada ya kusema hayo niwakumbushe tu kwamba wiki iliyopita tulishuhudia Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akivalia njuga wizi unaofanyika katika bandari yetu ya Dar ambayo ni moja ya vinu vinavyozalisha fedha hapa nchini.

Viongozi hao waligundua kuwa kulikuwa na makontena 349 yalitolewa bandarini kwa njia za panya na kuisababishia hasara serikali ya shilingi bilioni 80!

Ni jambo zuri kwamba viongozi wao wakuu wa serikali walifikishiwa kashfa hiyo nzito ambayo inafanywa na viongozi wenye dhamana katika nchi hii.

Niliwahi kusema huko nyuma kwamba kuna tabia hapa nchini, mtu akishaingia serikalini na kuwekwa sehemu yenye fedha, akaiba fedha za umma na kujenga mahekalu pia kununua magari ya kifahari, wananchi wanamuona mtu huyo ana akili sana.

Mbaya zaidi utakuta mtu na akili zake anamsifu mtu kama huyo kwamba eti mwerevu kwa sababu ndani ya mwaka mmoja kajenga mahekalu, kanunua magari ya kifahari na ana siha njema!

Sifa hizo za kijinga sasa zinapaswa kuachwa. Kila Mtanzania awe askari wa kulinda mali za umma. Inawezekana kabisa kwamba makontena hayo 349 yaliyotangazwa na Ikulu, siku za nyuma yangepita na wahusika kusifiwa mitaani kwa ‘werevu’ wao wa kuyapitisha bila kulipia ushuru.

Lakini naamini wapo raia wema waliijulisha Ikulu nayo ikafanya ilivyofanya na sasa tuna uhakika kuwa mabilioni hayo yaliyokuwa yaingie kwenye mifuko binafsi, sasa yataingia mfuko wa hazina na tutafaidi wote.

Huko nyuma tumeshuhudia kashfa za kutisha sana kama vile ya Epa, Tegeta Escrow, Meremeta, Kigoda, UPTL, mikataba ya madini na kadhalika lakini hatujasikia hatua kali zikichukuliwa.

Kuwa na roho ya wizi na kutojiheshimu na kutowajibika kwa viongozi kwa wananchi kunaleta kutoheshimka kwa viongozi mbele ya jumuiya ya kimataifa na ni fedheha kwa wananchi wanaowaongoza.

Mwalimu Julius Nyerere aliheshimika na wananchi au hata na mataifa ya nje siyo tu kwa kuwa alikuwa mkali bali kwa kuwa aliheshimu dhamana ya kuongoza nchi aliyopewa na wananchi.

Na ndiyo maana siku aliyofariki dunia watu bila kujali itikadi na dini zao, watu walimlilia sana kwa kuona kuwa alikuwa mtetezi wa wanyonge.

Wizi wa waziwazi unaofanywa na watu tunaowapa dhana ni ishara za dhahiri kwamba viongozi wetu sasa hawajiheshimu.Tumewahi kushuhudia baadhi ya vigogo wakituhumiwa kuhusika na rushwa na ufisadi wakakimbilia kujisafisha mahakamani.

Lazima tukiri kwamba sheria zetu ni dhaifu ndiyo maana watu wanaiba mali za umma bila woga wowote. Ni lazima sasa sheria hizo ziwe kali ili watu wanaoiba wakithibitika mahakamani basi wajutie na wale waliokuwa na nia ya kuliibia taifa waogope kufanya hivyo.

Siwezi kusema ni adhabu gani wapewe lakini wabunge, hasa bunge la mwaka huu ambalo limejaa wasomi watakuwa na uchungu na nchi yetu na kuhakikisha wezi wa mali za umma, hawasalimiki mahakama inapowatia hatiani.

Hatima ya uchumi na maendeleo ya nchi sasa haitabiriki maana mali ya umma imegeuzwa shamba la bibi lakini kwa hatua hizi za Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa, Watanzania tunaanza kuona mwanga.

Kila mtu awe adui wa mwizi wa mali za umma.MUNGU hapendelei ndiyo maana wote katuumba tuishi kwa kuvuta hewa ileile, miili yetu wanadamu wote ni sawa, mifupa na grupu za damu zetu ni sawa, awe Mzungu, Mwarabu, Mhindi, Mwafrika, au chotara, hivyo tumhimidi daima.

Baada ya kusema hayo niwakumbushe tu kwamba wiki iliyopita tulishuhudia Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akivalia njuga wizi unaofanyika katika bandari yetu ya Dar ambayo ni moja ya vinu vinavyozalisha fedha hapa nchini.

Viongozi hao waligundua kuwa kulikuwa na makontena 349 yalitolewa bandarini kwa njia za panya na kuisababishia hasara serikali ya shilingi bilioni 80!
Ni jambo zuri kwamba viongozi wao wakuu wa serikali walifikishiwa kashfa hiyo nzito ambayo inafanywa na viongozi wenye dhamana katika nchi hii.

Niliwahi kusema huko nyuma kwamba kuna tabia hapa nchini, mtu akishaingia serikalini na kuwekwa sehemu yenye fedha, akaiba fedha za umma na kujenga mahekalu pia kununua magari ya kifahari, wananchi wanamuona mtu huyo ana akili sana.

Mbaya zaidi utakuta mtu na akili zake anamsifu mtu kama huyo kwamba eti mwerevu kwa sababu ndani ya mwaka mmoja kajenga mahekalu, kanunua magari ya kifahari na ana siha njema!

Sifa hizo za kijinga sasa zinapaswa kuachwa. Kila Mtanzania awe askari wa kulinda mali za umma. Inawezekana kabisa kwamba makontena hayo 349 yaliyotangazwa na Ikulu, siku za nyuma yangepita na wahusika kusifiwa mitaani kwa ‘werevu’ wao wa kuyapitisha bila kulipia ushuru.

Lakini naamini wapo raia wema waliijulisha Ikulu nayo ikafanya ilivyofanya na sasa tuna uhakika kuwa mabilioni hayo yaliyokuwa yaingie kwenye mifuko binafsi, sasa yataingia mfuko wa hazina na tutafaidi wote.

Huko nyuma tumeshuhudia kashfa za kutisha sana kama vile ya Epa, Tegeta Escrow, Meremeta, Kigoda, UPTL, mikataba ya madini na kadhalika lakini hatujasikia hatua kali zikichukuliwa.

Kuwa na roho ya wizi na kutojiheshimu na kutowajibika kwa viongozi kwa wananchi kunaleta kutoheshimika kwa viongozi mbele ya jumuiya ya kimataifa na ni fedheha kwa wananchi wanaowaongoza.

Mwalimu Julius Nyerere aliheshimika na wananchi au hata na mataifa ya nje siyo tu kwa kuwa alikuwa mkali bali kwa kuwa aliheshimu dhamana ya kuongoza nchi aliyopewa na wananchi.

Na ndiyo maana siku aliyofariki dunia watu bila kujali itikadi na dini zao, watu walimlilia sana kwa kuona kuwa alikuwa mtetezi wa wanyonge.
Wizi wa waziwazi unaofanywa na watu tunaowapa dhana ni ishara za dhahiri kwamba viongozi wetu sasa hawajiheshimu.

Tumewahi kushuhudia baadhi ya vigogo wakituhumiwa kuhusika na rushwa na ufisadi wakakimbilia kujisafisha mahakamani.

Lazima tukiri kwamba sheria zetu ni dhaifu ndiyo maana watu wanaiba mali za umma bila woga wowote. Ni lazima sasa sheria hizo ziwe kali ili watu wanaoiba wakithibitika mahakamani basi wajutie na wale waliokuwa na nia ya kuliibia taifa waogope kufanya hivyo.

Siwezi kusema ni adhabu gani wapewe lakini wabunge, hasa bunge la mwaka huu ambalo limejaa wasomi watakuwa na uchungu na nchi yetu na kuhakikisha wezi wa mali za umma, hawasalimiki mahakama inapowatia hatiani.

Hatima ya uchumi na maendeleo ya nchi sasa haitabiriki maana mali ya umma imegeuzwa shamba la bibi lakini kwa hatua hizi za Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa, Watanzania tunaanza kuona mwanga. Kila mtu awe adui wa mwizi wa mali za umma.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Comments are closed.