The House of Favourite Newspapers

Abiria Wafurika Ubungo, Kwenda Mikoani Kula Sikukuu

ubungo-1

Mkuu wa kitengo trafiki wa Kituo cha Mabasi cha Ubungo, Mkaguzi wa Polisi, Ibrahim Samwix akiwa chini ya basi liendalo mikoani wakati akilikagua kabla ya kuondoka stendi hapo.

ubungo-2

…. Mkaguzi wa Polisi, Ibrahim Samwix akiliendesha basi kwa nia ya kulikagua kabla ya kuondoka mapema leo.

ubungo-3

…Mabasi yakindelea kukaguliwa kabla ya kuondoka.

ubungo-4

Baadhi ya abiria wakiwa stendi ya Ubungo mapema leo asubuhi.

ubungo-5

Abiria wakingojea mabasi Ubungo kuelekea kula Sikukuu za Krimasi na Mwaka Mpya mikoani.

ubungo-6

Mabasi ya daladala za muda zilizokuwa zikifanya shughuli zake katikati mwa Jiji la Dar es Salaam zilizopewa vibali vya muda kusafirisha abiria kuelekea mikoani zikiwa stendi ya Ubungo, Dar leo.

ubungo-7 ubungo-8 ubungo-9 ubungo-10

Abiria wakiwa wamefurika stendi ya Ungungo kusubiria usafiri kulekea mikoani.

ubungo-11

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, DCP Mohammed Mpinga (kushoto) akiwa ndani ya stendi ya Ubungo,Dar kuhakikisha abiria wanasafiri salama.

Na Denis Mtima/GPL

IKIWA imebaiki siku moja tu kufikia Sikukuu ya Krimasi, Kituo cha Mabasi cha ya Mikoani na Nje ya Nchi cha Ubungo jijini Dar es Salaam kimeonekana kufurika abiria baada kama mtandao huu ulivyonasa picha mbalimbali zinazoonyesha matukio yanayoendelea kituoni hapo.

Abiria wameonekana wakitafuta usafiri wa kueleka kusherehekea mikoani huku wengine wakiwa wamepumzika kusubiri mabasi.

Mtandao huu umeshuhudia mabasi kabla ya kutoka stendi kuu ya Ubungo kitengo cha Trafiki wa kituo hicho kinachoongozwa na Mkaguzi wa Polisi, Ibrahim Samwix kikikagua mabasi kabla ya kuondoka.

Comments are closed.