The House of Favourite Newspapers

Picha Iliyotingisha Facebook Mwezi Januari

 

mark-1

Mark Zuckerbeg (kulia) akiwa na mkewe jikoni. Angalia jinsi unga ulivyo tapakaa mezani…tehe …teheee!

Mwanzilishi wa kampuni ya Facebook, Mark Zuckerberg, Januari 27, 2017 aliweka picha mtandaoni sambamba na ujumbe ambao uliwagusa wengi katika kuchangia hoja zao.

Mark aliweka picha hiyo ikimuonesha yupo na mkewe jikoni wakiandaa chakula, picha hiyo iliwaonyesha wawili hao wakiwa na furaha huku wakiwatakia mashabiki wao heri ya mwaka mpya.

Ujumbe uliokwenda sambamba na picha hiyo uliandikwa:

“Happy Lunar New Year! Priscilla and I celebrated by making dumplings. I bet you can’t guess which ones were mine. Wishing everyone a great Year of the Rooster full of health, happiness, friends and family. 鸡年吉祥!”

Ujumbe huo ulipendwa na watu 977,000 na share 21,644 na waliochangia  ku-comment ni 23,328.

 

Salum Milongo/GPL

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Comments are closed.